Chama cha African National Congress (ANC), Afrika Kusini kimemchagua Cyril Ramaphosa, kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho akimrithi Jacob Zuma.
Ramaphosa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama tawala nchini Afrika Kusini ANC leo baada ya kufanyika uchaguzi.
Makamu huyo wa rais aliyeibuka mshindi alikuwa na upinzani mkali na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa Zuma.
Kulikuwa na mvutano, hisia zikipanda, wajumbe wakipiga kelele kupinga taratibu za upigaji wa kura.
Uwaniaji madaraka umeleta mvutano wa kisiasa nchini humo hali inayoleta hofu kuwa ANC inaweza kugawanyika kabla ya uchaguzi wa 2019.
Ramaphosa ameibuka mshindi kwa kupata kura 2,440 huku mpinzani wake Dlamini-Zuma akipata kura 2,261