Msigwa Aomba Nyumba yake Ichomwe Moto Kama Atahamia CCM

Mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa amewataka wananchi wa Iringa Mjini kumchomea nyumba anayoishi pamoja na magari yake endapo atahama Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kuhamia CCM.

Msigwa amefunguka hayo wakati akituma salamu kwa wale ambao wamekuwa wakimrubuni kuhamia CCM na kusema kwamba heshima na dhamana aliyopatiwa na wananchi wa Manispaa ya Iringa ni kubwa mno hivyo kufanya hivyo ni kuuza hadi utu wa wapiga kura.

Msigwa ameweka wazi kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka upande wa chama tawala wakimtaka akubali kupokea ofa yao ya kuhama chama na bila hivyo basi hataweza tena kurudi bungeni baada ya kufika 2020.

"Nikihamia CCM wananchi wa Iringa wachome nyumba yangu  na magari yangu. Sikuingia bungeni kwa sababu nataka hela ila nimeingia kwa sabu kuna hoja kuna agenda na kozi kama chama tunapigania.  Mkome kabisa kunipigia simu mimi sina bei itakayonihamisha CHADEMA," amefunguka Msigwa

Akizungumzia kuhusu alivyokuwa akirubuniwa, Msigwa amesema "Walianza kunipigia kwa kujifanya marafiki zangu na baadae wakaanza kunipanga na kunirubuni kwamba Mzee ananikubali na wala hana shida na mimi hivyo nikiingia CCM nitapata nafasi, nimewakemea na nimeonya wasinipie simu na sasa hivi wameacha ila naahidi wakinipia tena nitawarekodi niwaanike hadharani" I am not that 'cheap' wakatafute wengine," Msigwa ameweka wazi

Aidha Msigwa amefafanua kwamba hakuuingia bungeni kwasababu anahitaji pesa kwani hata kama asingekuwa Mbunge angeweza kuwa Mkurugenzi wa makampuni na kuongeza kwamba  alikuwa na maisha hata kabla ya kuwa mwanasiasa na mbunge.

"Sikuingia Bungeni kwa ajili ya pesa, sipo tayari kurubuniwa kwa maneno matamu wala fedha au ushawishi kuuza utu ambao wananchi wa manispaa ya Iringa wamenipa. Ukiniangalia kwani nashindwa kuwa CEO, naweza kuwa Mkurugenzi wa kampuni yoyote. Mimi nilikuwa na maisha kabla ya kuingia hta bungeni.  Sisi bado tupo imara....wacha hivi vivulana viondoke sisi ambao tunajua nini tunakutaka bado tupo imara ndani ya chama" Msigwa.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndo maneno yenu tumeyazoea.

    ReplyDelete
  2. Msigwa huna ata Haya....!!!
    Hii siyo olijino.... Umekopi ya Kujitakia Majanga.... Original yule wa Tanga sijui Muheza
    Hata hii Umedandia....
    Hovyooooooo..............!!!!!

    ReplyDelete
  3. Hivyo wewe unajiona Unahazi ya Kuingia CCM...???
    Unafikiri Pole Pole atakukubali? Labda Lema..
    Kwa wewe Sizani.... Hata hapo ulipo sijiu kama wanafaida na wewe..... Kulikoni Msigwa??
    Kama unafikiri utakatiwa Mgao wa Posho.(Umepiga Chini) zina wenyewe kina Edo / Baba Zero na Mtowe.

    unasikitisha hata unavyo zungumza Nakuoneaga Huluma Mwanangu.

    Tena nasikia Hii ndiyo awamu yako ya Mwisho kama utamaliza. Huo mjini unawenyewe na wananchi wameshastukia Picha.
    Poleni sana.

    ReplyDelete
  4. Mdau, Umenikosha..!! Kweli Original mwenyewe ni Silinde wa Mombo ( Sasa huko huko Tamga).
    Huyu nae si wale wale.... Kiboko yake Lusinde na Humphrey...!!!

    Spidi ya JPJM imewaacha Hoi Bin Taabani.... Hawajielewi Kabisa.

    Hapa Kazi Tu.

    ReplyDelete
  5. Eeeeeehhhhh Makubwa Haya ndugu zanguni.
    Kavaa kama suti vile nyeusi.
    Nilikutana nae Kihesa, Anakama kuchanganyikiwa vile.
    Hajui ashike neno la Bwana au aendelee na free Mani.

    ReplyDelete
  6. Hivi Msigwa tayari mlishapimana akili kwenye chadema? Maana ulisema atakaye mpokea Lowasa akapimwe akili......hii kauli itakuganda mpaka mkapimwe kweli, vinginevyo 2020 mtaisoma namba........

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad