Msigwa Awavaa Viongozi wa CCM

Msigwa Awavaa Viongozi wa CCM
Mbunge wa Iringa Mjini  CHADEMA, Peter Msigwa amewavaa baadhi ya viongozi wa CCM ambao wamekuwa wakisema upinzani Tanzania unakufa na kuwahoji kuwa endapo upinzani ukifa ndiyo maendeleo ya nchi yatapatikana.

Msigwa amesema hayo jana kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya juzi baadhi ya viongozi wa CCM waliokuwepo kwenye Mkutano Mkuu UVCCM wa 9 ambao ulifanyika mjini Dodoma Disemba 10, 2017 ambapo wapo baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho walikuwa wakisema kuwa kwa sasa upinzani nchini unakufa.
"Mkutano wa UVCCM ulibebwa na kibwagizo cha upinzani kuwa unakufa ! Fine, tukubaliane kuwa upinzani unakufa! Ukifa upinzani zitaongezeka ajira ngapi! Umaskini utapungua kwa kiwango gani? Haki za binadamu zitalindwa kwa kiwango gani? Utawala bora utaimarika kwa kiwango gani ? Demokrasia itaimarishwa kwa kiwango gani? Uhuru wa kutoa mawazo na vyombo vya habari utaimarika kwa kiwango gani! Haya yote hayana chama! Nilitegemea CCM mje na majibu ya haya sio upinzani unakufa" alisisitiza Msigwa
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hebu msiji-sahaulishe, hivi mlishapimwa akili? Maana ulisema atakaye mpokea Lowasa akapimwe akili!! tehe-tehe-tehe naona zako ndio zinazidi kuvurugika, mpaka ukapimwe-SHUBAMITTT!

    ReplyDelete
  2. Jamani .... Hapa kweli tunaupinzani?????
    si inasikitisha ukisoma hii.....
    Sina hata La zaidi.....
    Hivyo nini kimewasibu hawa Vijana na kukosa Hoja na Mwelekeo... Au siasa za kuokota zimekwisha??

    Tena wote Pwaaaaaaaaaaaaaa.....!!!!!! Msigwa na wewe uko Njiani? Kama Lemwa.?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad