Mtandao wa Facebook Waingia Kwenye Mtihani Mkubwa Watakiwa Kutoa Taarifa za Watumiaji Wake

Mtandao wa Facebook Waingia Kwenye Mtihani Mkubwa Watakiwa Kutoa Taarifa za Watumiaji Wake
Mtandao wa Facebook unapambana na changamoto ya kutakiwa kutoa taarifa za watumiaji wake kutoka katika mamlaka mbalimbali duniani.

Ingawa mtandao huo kuna baadhi ya taarifa hauzitoi, idadi ya maombi ya taarifa imeongezeka ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita.

Marekani, India, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zinaongoza kwa kuomba taarifa za watumiaji ikiwa ni asilimia 73 ya maombi yote yanayotumwa.

Hata hivyo, wakati mamlaka zikiongeza maombi, Facebook nao wameongeza orodha ya taarifa ambazo hawawezi kuzitoa.

Zipo taarifa ambazo Facebook kabla ya kuzitoa humtaarifu muhusika lakini zipo ambazo zinatolewa bila mhusika kujulishwa.

“Asilimia 57 ya taarifa zilizoombwa na mamlaka za Marekani hazikuturuhusu kuwataarifu wahusika, ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 ukilinganisha na mwaka jana,” anasema Makamu Kansela wa Facebook, Chris Sonderby.

Mbali na maombi hayo ya mamlaka, Facebook pia imefungua milango ya maombi ya uwajibikaji katika taarifa zinazowekwa katika mtandao huo.

Katika kipindi cha mwaka mmoja jumla ya maombi zaidi ya  200,000 yalitumwa wakihusiana na taarifa za wizi wa hakimiliki na asilimia 68 ya kazi hizo ziliondolewa katika mtandao huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad