Wanakijiji wakishirikiana na familia husika walifanikiwa kuokota mabaki ya mwili wa mtoto huyo yakiwamo utumbo na kipande cha mfupa wa ambavyo vilizikwa kwa heshima kijijini Buzanaki na tayari fisi saba wameuawa katika nyakati tofauti katika oporesheni ya kuwasaka.
Ofisa wanyamapori wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Msese Kabulizina, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 2, mwaka huu zikiwa ni siku tatu tangu wakazi wengine wa Kijiji cha Idoselo Kata ya Luezela wilayani Geita nao kujeruhiwa na fisi kisha kulazwa katika Hospitali ya Rufani ya mkoa wa Geita.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Desemba 2,wakati akitoka kuchuma embe zikiwa ni siku mbili tu baada ya wakazi wengine watatu wakazi wa kijiji tofauti cha Idosero Kata ya Luezera kujeruhiwa na fisi.
Walwa aliongeza kuwa tukio la kujeruhiwa watu watatu lilitokea usiku wa kuamkia Novemba 29 usiku baada ya kundi la fisi wanaodaiwa kuwa zaidi ya wanne kuvamia nyumbani kwa mzee Magadula kisha kuishambulia familia hiyo kabla majirani kufika kutoa msaada na wao kujeruhiwa.
Aliongeza baada ya fisi hao kuvamia ndipo familia hiyo ilipopiga makelele kuomba msaada na majirani waliofika kwanza walikuwa ni Kulwa Jamoka na mwanaye Yohana Kulwa ambao katika kutoa msaada nao walijikuta wakijeruhiwa.
Hata hivyo, wakati makelele yakiendelea huku fisi nao wakishambulia wao na mbuzi nakumtafuna kabla ya umati wa wanakijiji kuongezeka na kuanza msako ambapo hadi Jumamosi walikuwa wameuawa fisi saba katika matukio tofauti kwa kusaidiana Idara ya Askari wanyamapori Halmashauri ya wilaya ya Geita.