Mtuhumiwa wa Mauaji Ajilipua Wakati wa Kesi Yake Ikiendelea Mahakamani

Mtuhumiwa wa Mauaji Ajilipua Wakati wa Kesi Yake Ikiendelea Mahakamani
Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji amejilipua kwa kutumia maguruneti mawili katika mahakama moja mashariki mwa Ukraine.

Mtuhumiwa huyo amejilipua yeye na mtuhumiwa mwenzie wakati kesi yao ya kuua kwa kukusudia ikisikilizwa katika mahakama mjini, Nikopol katika jimbo la Dnipropetrovsk, Ukraine.

Kwa mujibu wa Polisi mjini Nikopol wamesema watu wawili wamefariki dunia na tisa kujeruhiwa kwenye tukio hilo wakiwemo washtakiwa wawili , walinzi wawili na mawakili watatu wa serikali na raia wawili waliokuywa wanasikiliza kesi mahakamani hapo.


Ndani ya mahakama hiyo baada ya mlipuko kutokea.

Mtuhumiwa huyo na wenzake watatu wanatuhumiwa kulifyatulia risasi gari moja na kuwaua abiria wawili mnamo mwezi Februari 2016.

Kwa mujibu wa mtandao wa Ukrainska Pravda taarifa zinasema mtuhumiwa mmoja alitoa maguruneti mawili wakati kesi ikiendelea mahakamani hapo na kuyalipua.

Gazeti hilo likimnukuu Msemaji wa Jeshi la Polisi mjini Nikopol, Yaroslav Trakalo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alichukua hatua hiyo baada ya kusikia kwamba kesi hiyo inaahirishwa na kwamba watuhumiwa wanarudishwa rumande.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad