Mume, Mke Wafikishwa Mahakamani kwa Kosa la Kusafirisha Dawa za Kulevya

Mume, Mke Wafikishwa Mahakamani kwa Kosa la Kusafirisha Dawa za Kulevya
Wafanyabiashara watatu kati yao wawili wakidaiwa kuwa mume na mke, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa kusafirishaji dawa za kulevya aina ya Heroin ya gram 375.20.

Washtakiwa hao ni Minda Mfamai, Fatuma Mpondi na Oswini Mango. Kwa pamoja wamesomewa makosa yao na Wakili wa serikali, Adolf Mkini mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Wakili Mkini alidai washtakiwa wanakabiliwa na kosa la usafirishaji wa dawa za kulevya aina Heroin zenye uzito wa gram 375.20. Inadaiwa walitenda kosa hilo November 22, 2017 maeneo ya Chamazi kwa Mkongo jijini Dar es Salaam.

Baada ya kusomewa kosa hilo, Hakimu Mashauri alisema washtakiwa hawapaswi kujibu chochote kwa kuwa kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi na mahakama hiyo haina mamlaka na kwamba kesi hiyo inapaswa kusikilizwa Mahakama Kuu, au hadi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) atoe kibali ndipo itaweza kusikilizwa.

Hata hivyo, mshtakiwa Mfamai aliiomba mahakama itoe amri akatibiwe kwa sababu amepigwa na polisi wakati akiwa kituo cha Polisi. Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri aliagiza mshtakiwa huyo na wenzake wakatibiwe ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi December 19, 2017.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad