Mwakani Naanza Kutoa Kazi Rasmi- Ferooz

Mwakani Naanza Kutoa Kazi Rasmi- Ferooz
Msanii Ferooz ambaye sasa anafanya vizuri na ngoma zake mbili 'Nakaza Roho' na 'Najaribu' amefunguka na kusema kuwa mwaka 2018 kwake ndiyo utakuwa mwaka rasmi wa kuanza kuachia kazi zake zilizopo ndani.


Ferooz akiongea na EATV Digital amesema kuwa saizi ameachia wimbo wake mpya 'Najaribu' kama zawadi kwa mashabiki wake kwa ajili ya Christmas na Mwaka mpya ila ataanza rasmi kuachia kazi zake mwakani 2018.

"Saizi nimewapa mashabiki zangu video mpya kama zawadi ya sikukuu ila kazi rasmi zangu zitaanza kutoka mwaka 2018, ambapo kazi yangu ya kwanza ambayo nitaachia mwakani nimewashirikisha Chege pamoja na Rich Mavoko. Kwa hiyo niwaambie tu mashabiki kuwa 2018 ninakuja na kazi za moto zaidi" alisema Ferooz
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad