Mwanafunzi Aliyepiga Picha za Nyufa Kwwenye Mabweni ya UDSM Akamatwa

Mwanafunzi Aliyepiga Picha za Nyufa Kwwenye Mabweni ya UDSM Akamatwa
Imeripotiwa kwamba Mwanafunzi aliyepiga picha na kuripoti nyufa kwenye majengo ya mabweni ya chuo kikuu cha Dar es salaam amekamatwa na polisi.

Taarifa za kukamatwa kwa mwanafunzi huyo ambaye pia ni kiongozi kwenye serikali ya wanafunzi ndg. Kumbusho Dawson zimethibitishwa na Makamu wa Rais (Daruso) Bi Anastazia Anthony ambaye amesema "Ni kweli na kwa sasa ndiyo  anapelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay. Asubuhi wanahabari walikuwepo hapa na hata watu wa TBA walikuwepo lakini baada ya kuondoka na yeye ndyo akaja kukamatwa"
Kwa mara ya kwanza na Mbunge Heche aliripoti habari hii akisema kwamba "Nimeambiwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi (Daruso) Kumbusho Dawson aliyeripoti nyufa kwenye majengo ya hostel za chuo amekamatwa na polisi!
Hata hivyo sababu za kukamatwa kwake bado hazijajulikana.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huwezi kuficha ubovu, ni bora kuweka wazi mapema ili kurekebisha kuliko kusubiri maafa.tumeona magorofa makubwa kuliko hayo mabweni lakini hayana nyufa. Nyufa inaelezea upungufu katika ujenzi. msione haya kukubali upungufu kuliko kusubiri maafa. kumbuka mficha maradhi..........!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad