Mwijage Ameitaka Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) Kubadilisha Mfumo wa Utendaji

Mwijage Ameitaka Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) Kubadilisha Mfumo wa Utendaji
WAZIRI wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, ameitaka Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kubadilisha mfumo wa utendaji ikiwa ni pamoja na kutoingia mikataba inayoweza kuisababishia serikali hasara, badala yake kuangalia wabia wanaoweza kuisaidia kujipanua na kupata faida kubwa zaidi.

Waziri Mwijage, aliyasema hayo juzi wakati akiizindua bodi mpya ya Wakurugenzi ya TFC, na kuongeza kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli, haiko tayari kuona taasisi zake za umma zikiingizwa katika mikataba mibovu na isiyokuwa na tija.

Pia aliagiza kwamba, baada ya kuizindua bodi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Egid Mbofu na wajumbe wake, waanze kazi mara moja na moja ya majukumu yao ya awali ni kuangalia ama kuipitia upya miokataba ambayo awalo iliingiwa na TFC.

Alisema TFC ikifanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kujielekeza kwenye kazi zenye faida kubwa, itaweza kusaidia kasi ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini, na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya Taifa la uchumi wa kati na wa Viwanda.

"Tunatambua sekta ya kilimo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uchumi wa TANZANIA, lakini haiwezi kuleta mafanikio makubwa kwa jamii, ikiwa TFC haitaweza kupewa uwezo na kuwafikia wakulima wengi zaidi", alisema Waziri Mwijage

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu waziri wa kilimo. Nilisoma miezi iliyopita kwamba kuna sera ya kutransform kilimo chetu na kukielekeza kwenye uzalishaji wa GMO. Ingawa mpango huo imefocus zaidi kt faida za GMO, umesahau kutizama madhara yake kiafya. Mfano soma www.diabeticconnect.com
    Ombi lang: hata km ndo The focus. Kilimo cha organic kuzingatiwe than before. La sivyo the negative effects of the GMO zisije kutufanya kujuta siku za using. Km tunaiga nchi zilizoendelea. Kt nchi hizohizo ni watu wenye kipato ndo wanaweza kuaford organic on daily basis. Wenye uwezo ndogo wao ni GMO na walio fukara zaidi ni vyakula vya makamo. Tafiti nyingi kt nchi zilizoendelea au za maendeleo ya viwanda zimeonyesha kuna tabaka kuu kiafya kati ya fukara na matajiri. Ingawa sababu haifahamiki, kuna connection kuu kat ya life style na health and illness including urefu wa muda wa kuishi. Naomba badala ya kufocus on GMO Tz iwe kinara wa kuzalisha organic na kuexport

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad