Ndugai Ametuma Salamu za Rambi Rambi kwa Waziri Ulinzi Kufuatiwa Kifo cha Askari wa JWTZ

Ndugai Ametuma Salamu za Rambi Rambi kwa Waziri Ulinzi Kufuatiwa Kifo cha Askari wa JWTZ
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ametuma salamu za rambi rambi kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, kufuatia vifo vya askari 14.

Spika Ndugai amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya askari hao ambao walikuwa wakilinda amani nchini Kongo, pamoja na wengine 44 waliojeruhiwa kufuatia mashambulizi yanayotekelezwa na askari waasi nchini humo.
Kufuatia tukio hilo, Spika Ndugai ametoa pole kwa familia za askari hao waliouawa, na kuwaombea wale waliojeruhiwa kupona haraka na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. poleni sana mashujaa wetu.
    kufaya kwenu ni heshima na ujasiri kwa nchi yetu.
    mungu awape subira na uvumilivu wana familia na wote tulioguswa na msiba huu WatanzaniaNa Serikali itafanya yote yali kuwa na owezo nao including kuwapa mafao na kusaidia kusomesha watoto wa Marehemu. ikiwemo serikali ya kongo piaMungu azilaze pema Roho zao.
    AMEENNNNNNN

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad