Ni kwa Nini Suti Bado Inapendwa Sana?

Ni kwa Nini Suti Bado Inapendwa Sana?
Katika mji wa London kuna duka la Henry Poole & Co lililo katika mtaa maarufu kwa suti za wanaume.

Kampuni hiyo ni tangu mwaka 1806. Miaka iliyofuatia mitido ya suti ya Uingereza ilipata umaarufu duniani.

Kufuatia bei ya suti ya Henry Poole & Co kuwa takriban dola 5,300, itakuwa rahisi kufikiria kuwa suti ni vazi la watu wa hadhi ya juu lakini meneja wa kampuni hiyo Simon Cundey hakubaliani na hilo.

Wanaume bado uhisi vizuri zaidi na wakiwa wametulia wakati wamevaa suti, na ufurahi pia wakiwa wamevaa vazi linalowatoshea vizuri.

Kwa Picha: Mitindo ya mavazi katika tuzo za Emmy
Watu wengi katika ulimwengu wa sasa wanashughuli nyingi na hawana muda mwingi wa kuingia duka hili au lile kujaribu kupata nguo ambayo inaweza kuwatoshea vuzuri.

Suti ni ghali lakini kama unaweza kuangaliwa gharama yake kwa miaka 10 ambao ni muda inaweza kudumu, basi hiyo inaweza kuwa sababu muafaka ya bei yake.

Suti imekuwepo tangu karne ya 17 na imekuwa ya mshono mmoja tangu mwanzo wa karne ya 20. Kuonekana kwake pia kumekuwa kwa nia moja kote duniani wakiwemo kwa watu wenye hadhi ya juu na wanaume wa kawaida, na hatimaye kwa wanawake ambao na wameanza kuvaa suti za aina tofauti.

Mkurugenzi wa taasisi wa mitindo mjini New York Valeria Steel, anaamini kuwa suti imedumisha nguvu zake.

Wanawake watakiwa kuvalia nadhifu Uganda
Kwa mtu ambaye anafahamu mawili au matatu kuhusu kuchimbuka kwa suti, ni mchora mitindo Sir Paul Smith ambaye amewavisha watu maaruuf kama Pink Floyd na David Bowie.

"Ninavaa situ kila siku, hata wikendi, anasema Smith. "Nimegundua kuwa zinanifanyia kazi nzuri sana, anasema akiwa kwenye studio

Martin Pel ambaye ni mwanamitindo huko Royal Pavilion eneo la Brighton anaitaja suti kuwa kitu cha kusawazisha. Suti inasabisha mtu kutofikiria hali ya mtu au anatokea wapi.

Akiguzia kazi ya Anne Hollander, Valerie Steele anasema kuwa moja ya sabubu ya suti kuwa maarufu kwa kupindi kirefu ni kuwa kwa ghafla imefanya mwili kuhisi shwari.

Wakati wa vita miaka arobiani wanawake walichukua nyadhifa za wanaume na kuanza kuvaa suti pia.

Wanaume walikuwa vitani ndipo wanawake wakapata fursa ya kuvaa suti, lakini hawakuvaa suruali bali sketi.

"Sidhani kama suti inaweza kutoweka anasema Martin Pel. Nafikiri kuwa ni nguo muhimu sana. Hata kama tutaivaa kila siku au wakati wa shughuli maalum suti haitatoweka.

Vile Paul Smith anasema: unaweza kwa na miaka 13 au 100 au mtoto wa shule lakini suti ni vazi bora
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad