Nuh Mziwanda Afungukaa Uhusiano Alionao na Shilole "Bado Naawasiliana Nae"

Nuh Mziwanda Afungukaa Uhusiano Alionao na Shilole "Bado Naawasiliana Nae"
Msanii wa muziki Bongo, Nuh Mziwanda amesema bado anawasiliana na aliyekuwa mpenzi wake, Shilole.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Bao la Ushindi’ amesema huwasiliana iwapo kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

“Kwa sababu sisi ni binadamu, kuna kuumwa, kuna misiba kwa hiyo utashindwa kwenda kwenye msiba kwa sababu ninyi mlikuwa mmeachana ni vitu ambavyo havileti maana” Nuh ameiambia Bongo5.

“Mimi sina noma, hata sign ya studio yangu ukisikia nyimbo zangu hizi mpya za sasa hivi Bao la Ushindi, Anameremeta ni sauti yake. Kwa hiyo tupo kikazi kama tulivyofanyaga tour ile ni kazi, ikitokea tunafanya” amesema.

Shilole amefunga ndoa hivi karibuni na mpenzi wake, Uchebe na baada ya hapo Nuh alitoa kauli ambao ilitafsiriwa kama amerusha dogo katika ndoa hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad