Nyalandu Augeukia Umoja wa Mataifa Sakala la Watumwa Libya

Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa wa Singida Kaskazini aliyejiuzulu, Lazaro Nyalandu ameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua zaidi juu ya kinachoendelea nchini Libya.

Mh. Nyalandu amesema kwamba ni lazima hatua zichukuliwe kwa kile kinachoendelea nchini Libya kwa vile  kinachoshuhudiwa kwa sasa ni matusi kwa wanadamu.

Kupitia kwenye mtandao wake wa Twitter Mh. Nyalandu ameandika
"Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika lazima uchukue hatua dhidi ya Libya sasa. Tunachoshuhudia ni matusi kwa wanadamu" Nyalandu

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zikiripotiwa kutoka Libya kwamba kumekuwa na biashara ya utumwa ikifanyika ikihusisha Libya kuuza waafrika wengine nchi za Ulaya.

Siku ya jana Ubalozi wa Libya nchini Tanzani umesema Waafrika wanaosemwa wanauzwa kutoka Libya, yawezekana walikuwa wanakabidhiwa kwa watoroshaji ili wawapeleke Ulaya na sio kuwauza kama watumwa.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie Waandishi Uchwara......Hiki kichwa cha Habari

    " Nyalandu Augeukia Umoja wa Mataifa Sakala la Watumwa Libya"

    Mmekitoa wapi na hiyo barua amempelekea nani? na ametumia njia gani ?
    Manayake havieleweki hivi mnavyo viandika.
    Nyalandu anafanya kazi wapi na kwa wadhifa upi?

    Umakini katika habari na vichwa vyake ni MUHIMU na inataka Weledi.

    Wanahabri Oyeeeeeeee..... Mwakyembe Oyeeeeeeee..... Tanzania Oyeeeeeee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad