Mh. Nyalandu amesema kwamba ni lazima hatua zichukuliwe kwa kile kinachoendelea nchini Libya kwa vile kinachoshuhudiwa kwa sasa ni matusi kwa wanadamu.
Kupitia kwenye mtandao wake wa Twitter Mh. Nyalandu ameandika
"Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika lazima uchukue hatua dhidi ya Libya sasa. Tunachoshuhudia ni matusi kwa wanadamu" Nyalandu
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zikiripotiwa kutoka Libya kwamba kumekuwa na biashara ya utumwa ikifanyika ikihusisha Libya kuuza waafrika wengine nchi za Ulaya.
Siku ya jana Ubalozi wa Libya nchini Tanzani umesema Waafrika wanaosemwa wanauzwa kutoka Libya, yawezekana walikuwa wanakabidhiwa kwa watoroshaji ili wawapeleke Ulaya na sio kuwauza kama watumwa.