Msanii wa muziki, TID amedai nyimbo za wasanii wa zamani zilikuwa zinadumu muda mrefu zaidi kutokana na wasanii hao kutumia muda mwingi zaidi kuandaa nyimbi zao.
Muimbaji huyo amedai nyingi za siku hizi zinashindwa kufanya vizuri na kudumu kutokana na kuandikwa kiwepesi wepesi.
“Nyimbo nyingi za zamani tulikua tunatumia muda kuandika pia hata waandaji wanafanya ‘mixing’ vizuri tofauti na ngoma za siku hizi zina copy kutoka nje ndio maana hazidumu” TID alikiambia kipindi cha Ladha 3600.
TID amesema wasanii wanatakiwa kuacha kucopy nyimbo za nje ili muziki wa Tanzania uendelee kukuwa.