Muuu wa wilaya ya Bunda mkoani Mara, Bi. Lydia Bupilipili ameliagiza jeshi la polsi wilayani humo kuendesha msako wa watu wanaofanya biashara ya ukahaba nyumba kwa nyumba.
Bi. Bupilipili ametoa agizo hilo katika kijiji cha Kunzugu alipokuwa anazungumza ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi wilayani humo, ambayo pia iliadhimishwa kwa kupanda miti.
Mkuu huyo wa wilaya amewataka polisi kupita nyumba kwa nyumba kwenye nyumba za wageni, na kuwasaka wanawake ambao wanadaiwa kukodisha nyumba hizo kwa ajili ya kuendesha biashara za ukahaba.
Miaka ya nyuma kulikuwa na zoezi la nguvu Kazi. Ukikamatwa tu unazurura unapelekwa moja kwa moja kijiji cha gezaulole na unakabidhiwa ardhi ili uwe mkulima na uachane kabisa na uzururaji. Wengi walinufaika katka hilo. Zoezi la kupunguza au kuzuia ukahaba likiwa constructive km lilivyokuwa lile la nguvu Kazi Itapendeza
ReplyDelete