Papa Francis Awataka Wakatoliki Kuwakumbuka Wahamiaji

Papa Francis amewahimiza waumini wa kanisa la Roma Katoliki wasiwatupia mgongo mamilioni ya wahamiaji ambao wamefukuza kutoka makaazi yao wakati wa misa kabla ya Krismasi

Kiongozi huyo wa dini aliwafananisha wahamiaji na Maria na Yosefu kutoka Bibilia, na namna ambavyo walivyosafiri kutoka Nazareti hadi Bethlehemu bila kupata makazi.

Papa Francis awataka makasisi Nigeria wamtii
Alieeleza kuwa wahamiaji wengi wanalazimika kukimbia viongozi wao ambao 'hawaoni tatizo na kumwaga damu ya wasio na hatia"

Papa Francis amefanya uteteaji wa wahamiaji kama maadhui yake kuu katika uongozi wake.

Image caption
Waumini wakiwa kwenye kanisa huko Bethlehem
Idadi ya wakimbizi duniani imezidi milioni 22,ikiwa idadi kubwa ikitokea kwa warohingya kukimbia uhalifu nchini Myanmar.

"Nyayo zao zimefichwa kwenye nyayo za Yosefu na Maria,' alielezea Papa Francis, ambaye yeye pia ni mjukuu wa wahamiaji kutoka Italia, kwa washirika wa kanisa la St Peters mjini Vatican,jioni ya Jumapili.

Papa amtimua kiongozi wa dini kwa kusambaza kondomu
Kiongozi huyo wa waumini waroma katoliki takriban bilioni 1.2 amesisitiza kuwa imani yao inataka wageni wakaribishwe kila mahali.

Papa Francis anatarajiwa kutoa hotuba yake ya "Urbi et Orbi" , yaani "kwa mji na kwa dunia" siku ya Jumatatu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad