Penzi kwa Simu Linanoga, ila Nikimuona Penzi Nywiii

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24 naishi Dubai. Nimepata Mchumba ana umri wa miaka 37 na kakubalika nyumbani na tuko kwenye harakati za kufunga Ndoa.


Kwakweli huyu bwana ananipenda sana kupita kiasi . Ananijali na kunithamini na kuniongoza katika kila jambo na kunishauri mambo yake yote kuhusu maisha yake na kwa kila kitu kiasi ambacho kanisubiri muda wa Miaka mitano ili nimalize masomo ili anioe.

Kwakweli miaka yote hatuna tabia ya kutoka pamoja wala kuonana ila nimazungumzo kwenye simu tu kwa muda wa miaka miwili.

Anakuja kwetu kawaida na mie kwakweli namempenda huyu kwa jinsi anavyonipenda na kunijali na navutiwa naye sana nikiwa naongea kwa simu kiasi ambacho siwezi kukaa siku bila kuongea nae na siwezi kufanya jambo bila kumshauri yeye tu.

Lakini cha kunishangaza akija kwetu kuonana na mie Moyo wangu unabadilika nahisi kuwa kama sijampendaa huyu mtu!

Naomba usinielewe vibaya  kusema kweli  nikikaa nikifikiria kiakili nahisi  sijaimpenda sura yake kwakweli na kwajinsi nilivyo huwa inanijia kama tukitoka wote itakuwa vipi?

Ila moyoni nampenda sana na siwezi kumkosa kabisa. Kwakweli nahisi nachanganyikiwa sijui nijiamulie vipi niufate moyo wangu au akili yangu?

Naogopa sana ikaja ikawa tatizo kwenye ndoa yangu na kutompa furaha anayoitarajia au je hili halitokuwa tatizo nikioana nae kwa vile Moyoni nampenda ntakuja kumpenda na kutojali sura yake.

Naomba Ushauri

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwanza kabisa acha kuzingua huyo jamaa hujampenda kabisa maana moyo ndo unatafsiri hisia zako sasa wewe sura umeionaje mbaya wakati una hisia nae? na kama unampenda na huwezi mkosa FUATA MOYO kama umalaya unakuzingua na huna hisia yeyote FUATA AKILI YAKO

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad