Penzi la Rayvany na Mpenzi Wake Bado Njiapanda Aamua Kumtumia Ujumbe Huu Mwanae

Penzi la Rayvany na Mpenzi Wake Bado Njiapanda Aamua Kumtumia Ujumbe Huu Mwanae
Staa wa ngoma ‘Mbeleko’ Rayvanny aliyeko Marekani kikazi, baada ya kurushiana maneno yaliyoashiria kuwa amekosana kimahusiano na mama wa mtoto wake,  ‘Fayhma’ sasa ameonesha kuelekeza mapenzi mazito kwa kinachoweza kubaki kama kumbukumbu isiyobadilika kama hawatamaliza tofauti zao kwa suluhu ya wawili hao kurudiana.

Akiwa mjini Washington, Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha ya mwanae, Jaydany sambamba na maneno yayoambatana kwenye picha hiyo yaliyozungumza kuutamani ukaribu wake na mtoto wake huyo. Bila shaka mapenzi ya mzazi na mtoto yamechangia kumsukuma Rayvanny aoneshe hisia hizo. Aliandika Hivi "miss u jayvannboy @jayvannyboy

Katika hilo la wawili hao kutokauwa katika hali nzuri ya kimahusiano, inahesabika kuwa ni miezi isiyopungua miezi 7 tangu wawili hao walipokaribisha mtoto wao huyo wa kwanza kwakuwa taarifa za wawili hao kupata mtoto zilisambaa tarehe 19 mwezi Aprili mwaka huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad