Polisi Wakumbana na Chatu Mkubwa Wakipiga Doria

Polisi Wakumbana na Chatu Mkubwa Wakipiga Doria
Maafisa wawili wa polisi katika jimbo Queensland nchini Australia walipigwa na butwaa walipokumbana na chatu mkubwa wakipiga doria.
Ingawa walipigwa na butwaa mwanzoni, walitumia fursa hiyo kupiga picha na chatu huyo.
Picha ya mmoja wa polisi hao ilipakiwa mtandaoni na imezua hisia si haba.
"Nyoka huyo alikuwa na urefu wa zaidi ya mita tano, na kusema kweli si kiumbe ambaye unaweza kutafuta utepe useme utampima," polisi hao waliambia BBC.
Wachezea nyoka kuajiriwa chuoni Nigeria
Nyoka atafuta 'joto' kwenye kiatu
Picha hiyo iliyopakiwa na polisi hao kwenye mitandao ya kijamii Ijumaa imetazamwa mara zaidi ya milioni mbili, na kutolewa maoni mara 10,000.

Polisi hao walikutana na nyoka huyo karibu na Wujul Wujul, karibu 345km (maili 210) kaskazini mwa jiji la Cairns.
Sumu ya nyoka ni dawa ya kumaliza uchungu
Kasisi aliyewalisha watu nyoka Afrika Kusini, afika Nigeria
Chatu aina ya Scrub, ambao huwa ndio nyoka warefu zaidi Australia, wanaweza kufikia urefu wa hadi 7m (futi 23).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad