Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu yaDar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kesi ya Dk Louis Shika hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba tatu za mfanyabiashara maarufu Said Lugumi alizoahidi kuzinunua zote zipo.
Novemba 9, 2017 kampuni ya udalali ya Yono kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliendesha mnada wa nyumba mbili za Lugumi zilizoko Mbweni JKT na moja Upanga jijini Dar es Salaam ambazo zote Dk Shika alifikia bei ya kuzinunua kwa Sh3.2 bilioni.
Mambosasa akizungumza leo Jumatano, amesema kesi yake haina mashiko hivyo hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba hizo zipo na hajatia hasara .
Amesema Dk Shika alikuwa akitamba kuwa ana fedha kumbe uwezo wake ni mdogo na kusababisha kushindwa kulipa asilimia 25 kwa kila nyumba hizo.
‘‘Dk Shika ni wa kumuonea huruma hana kitu tulisema tunamchunguza na tutampeleka mahakamani lakini tumeona kesi yake haina mashiko ndiyo maana hatuendelei nayo,” amesema Mambosasa.
Jeshi la polisi kanda hiyo lilimshikilia na kumwachia kwa dhamana Dk Shika ambaye alikuwa akituhumiwa kwa kuharibu mnada baada ya kushindwa kulipa asilimia 25 ya fedha hizo ambapo nyumba za Mbweni JKT alifika bei kwa Sh900 milioni na nyingine Sh1.1 bilioni, huku ya Upanga alifika bei ya Sh1.2 bilioni
kisamehewa Itapendeza.
ReplyDeleteTungoje aingize Mabilioni yake toka Thailand.
Huyu ni Shushu lakini baada ya KGB na CIA kuwa kwa sasa hawana mvutano kama wakati ulee.
Maisha yake hayana Tishio ila ni kwamba sasa Tumemuanika na anajulikana Pa Kupatikana Tafadhalini muwe mnamlinda hata kujua kila Jioni yuko Salama.
Mpeni hiyo kazi yeye mwenyewe awe anapiga simu namba maalum kwa miezi isiyo pungua Tisa, na Airport na land borders zote iwepo taarifa ya kuto toka ila kwa kibali maalum... hii ni kwa usalama wake.
Tisa Desemba Lazima Awe Dodoma ITAPENDEZA.... MWANGALUKA NGOSHA ....!!!!!