Polisi Yawaonya Madereva wa safari Ndefu

Polisi Yawaonya Madereva wa safari Ndefu
 Polisi Mkoa wa Pwani imetoa agizo kwa wamiliki wa magari yanayofanya safari ndefu kuzingatia uwepo wa madereva wawili.

Jeshi hilo limesema kinyume cha hilo, magari hayo hayataruhusiwa kuendelea na safari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shanna amesema hayo leo Jumanne Desemba 26,2017  akizungumzia namna walivyojipanga kidhibiti ajali.

Amewatahadharisha madereva wasio na uzoefu wa kwenda safari ndefu wasiendeshe magari ya abiria na badala yake watafute wazoefu ili kuepusha ajali zinazozuilika.

Amesema mwishoni mwa mwaka kumekuwa na ajali ambazo baadhi husababishwa na uzembe.

Taarifa ya Polisi Mkoa wa Pwani inaonyesha Januari hadi mwanzoni mwa Desemba mwaka huu matukio ya ajali yamepungua kutoka 396 za kipindi kama hicho mwaka jana hadi 98.

Kamanda Shanna pia ameonya wanaojihusisha na uhalifu na makosa mengine ya uvunjifu wa amani akisema wamejipanga kuwakabili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad