Kusimama majukwani tena madhabahuni kumkosoa Mkuu Wa nchi siyo njia sahihi na siyo njia ya staha kutumia!! Mkuu Wa dini anaheshimika na kila mtu hata Mungu anamheshimu sana tu!! Hivyo ukitaka kumuona Mkuu Wa nchi kwa lengo na kutaka kumhekimisha ( maana Kuhani au askofu anatakiwa awe na hekima ya kimungu ili kuwahekimisha wanadamu) sidhani kama utakataliwa pale ikulu kumuona mh rais! Kingine kulingana na katiba ya JMT mh rais halazimishwi mahala popote kufuata ushauri Wa MTU!!
Kiongozi Wa dini kuropoka hovyo juu ya Mkuu Wa nchi nikumkosea heshima muumba wako ,ni kuihalifu Biblia na maandishi matakatifu!! Hata Yesu huyo anayehubiriwa na wakuu Wa dini hakuwahi kuwakashfu wakuu Wa waserikali na ndiyo maana hata Pilato alikosa kosa la kumshitaki ndipo aliposema kuwa: sijaona hatia yoyote juu ya MTU huyu!! Haya yote ni kwa sababu Yesu au Issa Bin Mariam alihubiri njili ya amani yenye kuleta toba !!
Kiongozi Wa dini kazi yake ni kuhubiri njili ya amani iletayo toba ili watu waokoke!! Hakuna mahala popote Yesu alihubiri majukwani akimlazima Pilato au herode kuwa aokoke!! Mwenye heshima MPE heshima yake!Jifunzeni kwa Yohana mbatizaji alipojaribu kumkosoa Herode!! Njili ya Yohana mbatizaji ilikatizwa kwa kuchinjwa kichwa labda mahala pengine haikuwa sahihi kumkosoa hadhalani mfalme herode!!
Ukitaka kumhubiri Mkuu Wa nchi mwalike oficine kwako aanza kumhubiri!!
Ikulu ina tovuti ramsi ,mh rais ana email address kwa nini tusitumie njia hizi kutoa ushauri kwa rais! mh rais anayajua maovu ya kila mtu lakini hakuna mahala popote amewadhalilisha wakuu Wa dini kwa sababu anajua kwa kufanya hivyo atakuwa anagombana na Mungu !! Ikiwa anawaheshimu ninyi kwa nini msimheshimu?
Kazi ya Muumini na kiongozi wadini ni kuiombea serikali ikiyoko kadarakani regardless ni nzuri au mbaya!! Kuomba tu na siyo kuropoka majukwani!! Kuropoka majukwani ni dalili ya mtu aliyefilisika kiroho Sasa Anataka kupambana kimwili!! Biblia au Quran haijatufundisha kuwakashifu ,kuwakemea ,kuwatukana ,kuwakebehi ,kuwadhakilisha viongozi wetu!!!
Sasa wewe unatumia Biblia au Quran gani? Au umetunga Biblia au Quran ya kwako!!!
Umesomea wapi theologia mpaka kuwa askofu Wa kuwatukana watu? Au umesomea kuzimu kwa shetani ambaye ni mwasi tangia asili?? Lakini kama ulisomea kuzimu au shetani ndiye kakufundisha basi utashushwa mpaka kuzimu kama shetani alivyoshushwa mpaka kuzimu baada ya kuendesha uasi mbinguni!!
Tuwavumilie viongozi wetu kama vile tuwavumiliavyo waumini wengine Wa madhehebu yetu!! Muda wao wadarakani ni miaka mitano tu wakijitahidi ni miaka kumi!! Kwani kuleta matengano wakati kazi yetu ilitakiwa kuleta mshikamano?
Watanzania wa leo Sio wale wanauelewa.pole
ReplyDeleteSasa akosolewe wapi? kwa style gani?
ReplyDeletemikutano ya siasa imezuiwa, utasimama kwenye hadhara ipi umkosoe raisi? Binafsi sioni kosa la kakobe. kila mtu anao uhuru wa kusema lolote mahali popote pasi na kuvunja sheria. Rais ni mwanadamu kama mimi, akikosea lazima akosolewe na akubali kukosolewa. watu wasifungwe midomo.
Kwa vile kula ni lazima kwa binadamu, unadhani itakuwa sahihi ukenda kanisani na kiporo chako ukalia madhabahuni? I doubt about your logic and reasoning
Delete