Rais Magufuli Ameagiza Kuondolewa kwa Bodi ya Umoja wa Vijana UVCCM


Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli ameagiza kuondolewa kwa Bodi ya Umoja wa Vijana UVCCM kwa maelezo kuwa haina tija.
-
Aidha, ameagiza mali zote za UVCCM ziandikwe kwenye daftari moja ili iwe rahisi kwa ufuatiliaji.
-
Amewataka pia vijana wa CCM wasiwe waoga na wanyonge katika kujibu hoja za wapinzani wao wa kisiasa.
-
Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo mkoani Dodoma wakati akihutubia kwenye Mkutano wa 9 wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ambao unafanya uchaguzi wa kuchagua uongozi mpya huku Mwenyekiti wa Umoja huo, Sadifa Khamis akiwa mikononi mwa Polisi kwa tuhuma za Rushwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad