Rais Magufuli Atamani Kustaafu Urais "Natamani Nistaafu Niwaachie Wengine"

Rais Magufuli Atamani Kustaafu Urais "Natamani Nistaafu Niwaachie Wengine"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. John Pombe Magufuli amewatoa wasiwasi wananchi kwa kusema wazi kwamba anatamani siku moja ifike naye aitwe mzee mstaafu wa taifa hilo kama alivyo Kikwete na wengine.


Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua uchaguzi mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), maarufu kama NEC Taifa, mkoani Dodoma akiwakaribisha na kuwatambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wakiwemo Marais wastaafu.

''Natamani siku moja na mimi nistaafu, niitwe mzee mstaafu kama mzee Kikwete niwaachie wengine,'' amesema.

Vipindi vya ukomo kwa sheria iliyopo kwa nafasi ya Rais ni miaka 10 , sheria inaruhusu kila baada ya miaka mitano kufanyika kwa uchaguzi mkuu ili kuwapa demokrasia wananchi kuweza kuchagua kiongozi anayefaa.

Mwezi Julai, 2017 kuliibuka mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii kujadili kauli ya Rais mstaafu ya awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, aliyoitoa katika Baraza la  sikukuu ya Iddi aliyosema  kama isingekuwa matakwa ya kikatiba angetegemea kuona Rais aliyepo madarakani John Pombe Magufuli akipewa nafasi ya kutawala bila kikomo.

Mkutano huo wa leo utakipatia viongozi wapya wa ngazi ya juu chama hicho ikiwemo Mwenyekiti taifa na Mwenyekiti baraza la mapinduzi Zanzibar. Tayari Rais magufuli amethibitisha kuwa katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana ataendelea na nafasi yake.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Baba Usituvunje Moyo na Kuwapa Faida Maadui Zetu.
    Akasia watarudi kwa staili nyingine na Kutuibia Maradufu.
    Wauza Nchi wataiuza na Kutuuza sisi tukiwa Ndani yeke.
    Watoto zetu watakosa Elimu na Matibabu... Hali ya Kunyanyaswa Maofisini za Serikali itarudi.

    Baba chonde chonde usitoe mwanya wa Kuwapa Faraja Wabadhirifu na Mafisadi.

    Watasikia Raha na Kuanza kuota Ndoto Za Kihujumi na Kufikiria Mbinu mpya za Kuhujumu Nchi yetu na Kuvuruga Amani yetu.

    Kaza Buti utunyooshee nchi Hii na Kuileta Tanzania Mpya.

    Sisi Na Magu Na Magu na Sisi... Hatusikii lingine la Kishetani Mpaka 2027.
    Hapa Kazi TU. Milimonyi Muwaha.... mlungu akutaze mkuluuu...
    Karibu Dodoma
    Dodoma Yetu ni Safi na Ya Amani na Ni SALAMA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad