Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendesha harambee na kuchangisha jumla ya milioni 60 ambazo watapewa wajumbe wa Chama Cha Walimu ambao wamehudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu CWT.
Rais Magufuli alianzisha zoezi hilo kwa kutoa milioni 10 ili wajumbe hao waweze kupata fedha za chakula na baadaye Rais kuanza kuwaita viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi za Serikali ili waweze kuchangia fedha za chakula ambapo kwa ujumla ziliweza kupatikana jumla ya milioni 60.
Katika zoezi hilo la uchagiaji wa fedha hizo za chakula kwa wajumbe 1200 wa CWT lilikuwa kama ifuatavyo
Rais Magufuli milioni 10
Waziri Mkuu Milioni 10
Waziri wa Elimu, Ndalichako milioni 6
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama milioni 6
Mama Magufuli Milioni 1
Mama Majaliwa Milioni 1
Spika wa Bunge Job Ndugai Milioni 5
Katibu Mkuu Tamisemi Milioni 4
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Milioni 4
Mstahiki Meya wa Dodoma Milioni 1
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Milioni 1
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mstaafu) George Mkuchika Milioni 3
Mkuu wa Chuo cha Dodoma Milioni 4
Mkurugenzi wa usalama wa taifa Milioni 4
Jumla ya fedha zilizopatikana zilikuwa milioni 60 hivyo Rais Magufuli aliagiza kuwa milioni 50 wapewe wajumbe wa CWT huku milioni 10 zikienda kwa walimu wanafunzi wa UDOM ambao walishiriki katika Mkutano huo. Lakini pia Rais Magufuli aliagiza fedha hizo zifike kabla ya wajumbe hao hawajamaliza Mkutano wao.
Watanzania ni Wakarimu.
ReplyDeleteDodoma Ina Ukarimu wake.
Karibuni sana Kwi Dodoma
Mkulu wa'aza na Milimo Ilibah'oooo.
Mlungu wawataze!!!
Mulam'saje Wadodo Kukaya.... Mli waswano Du......
Tumefurahi kwa hili kongamano la walimu kuendelea Makao Makuuu
Karibuni sana kati hii awamu yetu ya Tano.
Hapa ni kazi Tuuuuuuuu.
Hapa milimo tu
ReplyDelete