Rais Magufuli awatoa wasiwasi Watanzania Kuhusu Ukomo wa Uongozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. John Pombe Magufuli amewatoa wasiwasi wananchi kwa kusema wazi kwamba anatamani siku moja ifike naye aitwe mzee mstaafu wa taifa hilo kama alivyo Kikwete na wengine.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua uchaguzi mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), maarufu kama NEC Taifa, mkoani Dodoma akiwakaribisha na kuwatambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wakiwemo Marais wastaafu.

''Natamani siku moja na mimi nistaafu, niitwe mzee mstaafu kama mzee Kikwete niwaachie wengine,'' amesema.

Vipindi vya ukomo kwa sheria iliyopo kwa nafasi ya Rais ni miaka 10 , sheria inaruhusu kila baada ya miaka mitano kufanyika kwa uchaguzi mkuu ili kuwapa demokrasia wananchi kuweza kuchagua kiongozi anayefaa.

Mwezi Julai, 2017 kuliibuka mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii kujadili kauli ya Rais mstaafu ya awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, aliyoitoa katika Baraza la  sikukuu ya Iddi aliyosema  kama isingekuwa matakwa ya kikatiba angetegemea kuona Rais aliyepo madarakani John Pombe Magufuli akipewa nafasi ya kutawala bila kikomo.

Mkutano huo wa leo utakipatia viongozi wapya wa ngazi ya juu chama hicho ikiwemo Mwenyekiti taifa na Mwenyekiti baraza la mapinduzi Zanzibar.

Tayari Rais magufuli amethibitisha kuwa katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana ataendelea na nafasi yake.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vuruga vichwa vya watu, badala ya kuwaongoza wananchi, kulinda mali zao, kuhakikisha na kuboresha amani. Hizi ndizo topic za maana kwa Watanzania , na Katiba iendanayo na wakati. Msilete maslaha kazini. Cheo ni dhamana, kila mtu amalizie yake.Mnatumia muda mwingi kuleta hadithi. Mnalipwa pesa nyingi kuwatumikia Wananchi. Ongeeni hoja zinazowasibu wananchi. Uhuru wa kufikuri na kutoa mawazo.ukweli, Usawa, heshima kwa wote, na unyeyekevu.Tumieni hekima.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad