Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni ameweka bayana kuwa katika miaka 30 iliyopita hajaugua ama kulazwa hospitalini na yote hiyo ni kutokana na kula mlo kamili lakini pia kutokunywa pombe.
Museveni ambaye ana miaka 73 ameiongoza Uganda kwa zaidi ya miaka 30 sasa na kwa muda huo wote amesema haijawahi kuripotiwa kuwa anaumwa kwa sababu hana muda na ugonjwa.
Museveni amesema kuwa serikali anayoiongoza imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha raia wa Uganda wanapata huduma bora za afya na kwamba walianza kwa kutoa chanjo za aina 8 na sasa wamefikia aina 13 ikiwemo chanjo ya Homa ya Ini aina B.
Rais Museveni ni kiongozi wa tatu Afrika ambaye hadi sasa yupo madarakani kwa muda mrefu zaidi ambapo wa kwanza ni Teodoro Obiang wa Equatorial Guinea, wa pili ni Paul Biya wa Cameroon.