Rais wa Zimbabwe Apiga Marufuku Nyimbo za Kumsifu na Kumtukuza

Rais wa Zimbabwe Apiga Marufuku Nyimbo za Kumsifu na Kumtukuza
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ametaka wanachama wa Chama cha Zanu-PF kuachana na nyimbo za kumsifu na kumtukuza.

Amewataka watilie mkazo wimbo wa Taifa na nyingine zinazozungumzia ukombozi.

Mnangagwa amesema hayo katika mkutano wa chama hicho uliomvua uongozi rasmi aliyekuwa kiongozi mkongwe wa chama na Serikali ya Zimbabwe, Rais Robert Mugabe na kumtimua mkewe Grace.

Mkutano huo pia umemwidhinisha  Mnangagwa kuwa mkuu mpya wa chama na mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2018.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mnangagwa amewataka wanachama kutambua kuwa yeye ni Rais wa watu wote na wala si wa kikundi fulani.

Amesema huu si wakati wa kutambiana kuwa kundi gani limeshinda bali kila mwanachama anapaswa kuzingatia mahitaji ya wananchi ambao wanataka maendeleo.

Rais Mnangagwa amesema wanachama wanapaswa kurekebisha uchumi ikiwa wanataka wawe na nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.

 "Tutashinda uchaguzi ikiwa tu tutaweza kuonyesha ishara kwamba tunafufua uchumi na wakati huohuo, tutaweza kupata mafanikio ya kiuchumi ikiwa tutaweza kuhakikisha tunashinda tena uchaguzi," amesema Mnangagwa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huu ndo uzalendo wa kweli. Anajijua na kujiamini. Anajua wengi waafrika hawana elinu sawasawa unaweza kumnadi kiongozi bila kumtukuza. Na anajua wimbo wa Taifa ndio kiungo kikuu cha watu kitaifa. Lakini kuna maraisi wengi wa Afrika wanapendwa kutukuzwa kila siku. Badala yake anakuwa kama ndiye Mungu na juu ya wote, badala ya kuwaunganisha Watu wote kupitia nembo ya Wimbo. Ni tofauti kielimu, na upeo wa fikra kujua nini ni muhimukwa Taifa. Ni Utaifa na si kiumbe. Kiumbe inambidi ajiegeze kwenye utaifa zidi ya chama, mtu, au hoja. Na watu wenye elimu za kubabaisha ni shida kujua hili. Ndo maana mataifa mengi ya Kiafrica, yanaupendeleo kindugu, kichama, kirafiki. Hizi ni tabaka ambazo zinaua utaifa. Na wananchi Wakielewa hili, haitakuwa shida kumuondoa raisi iwapo hatetei Taifa kwanza, haelimishi taifa, haunganishi Taifa. Utakuta mbomoko wa Taifa akiamini anachokifanya yeye ni bora na kifuatwe na kuunga mkono na wote, Kuna kuwa na uhaba wa kuelewa mambo. Na akizungukwa na watu kama yeye basi ni hatari kubwa. Ni hapa chanzo cha mtengano, na malimbwende kitaifa. Kisa, ujinga wa kutokuelewa lililoko mbele yake. Na vitu kama hivi vinahitaji Wananchi asilimia kubwa wawe na ujuzi na uwezo wa hali ya juu wa kuliona hili na kulitetea kwa hali na mali. Au la Taifa linaangamia bila kujijua. Sifa, na kutaka kukwezwa ndi hasa isababishayo kuto kujitambua.Nampongeza Huyu Raisi kwa hili. Ni mjasiri na mnyenyekevu, hataki kukupewa sifa ambayo ni majukumu yake ya kila siku kama kiongozi. Anatimiza majukumu aliyopewa na analipwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad