Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk Ali
Mohamed Shein, amewaonya wale waonadhani kuwa yeyeni mpole na kwamba
hawezi kuwachukulia hatua viongozi wa serikali na chama wanaovunja
nidhamu na kukiuka taratibu za utendaji.
Dk. Shein ambaye pia ni Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, ametoa kauli hiyo mjini Zanzibar katika sherehe za
kumpongeza baada ya kuchaguliwa tena kushika wadhifa wa Makamu
Mwenyekiti wa CCM katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa CCM uliofanyika mjini
Dodoma hivi karibuni.
Amesema, kiongozi wa nchi anapaswa kutumia taratibu za uongozi na si kukurupuka kwa kuwaadhibu watu bila ya utaratibu.
Amesema yupo madhubuti na imara kwa kuwashughulikia wanaovunja nidhamu ya chama hicho na hatomuonea wala kumuadhibu mtu bila kufuata utaratibu wa maadili ya CCM .
Amesema yupo madhubuti na imara kwa kuwashughulikia wanaovunja nidhamu ya chama hicho na hatomuonea wala kumuadhibu mtu bila kufuata utaratibu wa maadili ya CCM .