Nyota wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo anatarajia kujenga hospitali ya watoto jijini Santiago nchini Chile.
Hospitali hiyo ambayo itajengwa na Ronaldo akishirikiana na mfanyabiashara kutoka nchini Italia Alessandro Proto, inatarajiwa kukamilika kabla ya mwaka 2020.
Jiji la Santiago umekuwa mji wa kwanza kati ya mingine ambayo Ronaldo na Proto wanampango wa kujenga hospitali hizo za watoto barani Amerika Kusini.
Ronaldo amekuwa mdau mkubwa wa kuchangia damu kwaajili ya watoto wenye matatizo mbalimbali ambapo amefanya hivyo mara kwa mara. Pia nyota huyo ni balozi wa “Save the Children, Unicef “ na “World Vision”.
Mapema mwaka huu, Ronaldo alichangia kiasi cha £ 600,000 sawa na shilingi bilioni 1 milioni mia tano tisini na tano (Bil. 1,595/=), kwa ajili ya mpangoa wa kurudisha furaha kwa watoto maarufu kama “Make-A-Wish Foundation”. Fedha hizo zilipatika baada ya kuuza tuzo yake ya Ballon d’Or mwaka 2013.