Rosa Ree Afunguka Kuhusu Uwezo wa Harmorapa Kimuziki

Rosa Ree Afunguka Kuhusu  Uwezo wa Harmorapa Kimuziki
Msanii wa muziki Bongo, Rosa Ree amefunguka juu ya wale wanaoponda uwezo wa Harmorapa katika muziki.

Rapper huyo amesema ni vigumu kusema Harmorapa hana uwezo wa kimuziki ila kinachotakiwa ni yeye kuonyesha uwezo.

“Ni yeye kuendelea kuonyesha uwezo, huwezi kum-judge mtu kwa sababu ana sifa fulani mtaani au kwa sababu na muonekano fulani, kwa hiyo we can’t judge uwezo wa kipimo cha uwezo wa mtu ni bidii yake” Rosa Ree ameiambia Bongo5.

“Akitia bidii ndio inawezekana, mimi siwezi nikaja nikajiita rapper Rap Goddess wakati nyimbo ninazotoa ni mbovu, you have to call yourself what is your real hear, kwa hiyo ni yeye kuweka bidii anaweza kufika ninapotaka” amesisitiza Rosa Ree.

Kwa sasa Rosa Ree anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Dow’ baada ya kufunika vilivyo na ngoma ‘Up In The Air’.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Rosa ree Utaigiliaje anga za Wema..???
    Hamolapa kwa mdomo wake ametamka.. Wema amemzimilia.. Haji Manara ameshaombwa apunguze spidi zake.
    Hamolapa akishaweka ndani wema kiki itajipa Tuu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad