Rugemalila Aleta Mapya Mahakamani Anataka Kumtaja Mwizi wa Fedha za ESCROW

Rugemarila Aleta  Mapya Mahakamani  Anataka Kumtaja Mwizi wa Fedha za ESCROW
Mfanyabiashara James Rugemalila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anahitaji kuonana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili ampe ushahidi wa nani anayepaswa kukamatwa katika kesi hiyo.

December 8, 2017 Rugemarila aliieleza mahakama hiyo kuwa unahitajika ushirikiano baina yake na upande wa mashtaka ili kumbaini mwizi wa Sh.Bil 309 za Serikali.

Mbali ya Rugemarila, Mshtakiwa mwingine ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.

Rugemarila ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kudai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho.

Baada ya kueleza hayo, Rugemarila alinyoosha mkono ambapo amesema kuwa anaushukuru upande wa mashtaka ulimchukua gerezani na kumpeleka Upanga kwa mahojiano na kumrudisha salama gerezani.

“Leo nimekuja na ushahidi, hivyo naomba nikutane na DPP ili niweze kumsaidia kumjua mwizi anayepaswa kukamatwa, kwani lengo letu ni kuonyesha kuwa tupo Innocent,” alieleza Rugemarila.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi alimtaka Rugemarila kuwasiliana na mawakili wake ili waandike barua ya kuwasilisha kwa DPP kuhusu suala hilo la ushahidi wake, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 5, 2018.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duuu tutasikia mengi hila ikulu ilishasema fedha hizo sio za serikali

    ReplyDelete
  2. Rugemalila unaonesha ulikuwa mwana liaza.
    na Harbinder anaonesha alikuwa Kocha Mzuri.

    ReplyDelete
  3. Kama ni mtu wa IKULU mtaje basi.Innocent not Innocent hii ni nyingine. Mlilindwa Ikulu mnaogopa kuwataja. Wote mko hatiani. Ni vizuri uwataje wakuunge huko gerezani. Au mtaleta mchezo mwingine na kumaliza pesa za Watanzania. Ulishakingiwagwa kifua, ikashindikana. Kama ni yule unaogopa nini?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad