Sala ya Ukiwa Unamsikiliza Mpenzi Wako Akikudanganya Wakati Ukweli Unaujua


“Mungu baba uliyetuweka hapa duniani na kutupa kitabu cha kutuongoza katika njia iliyonyooka naomba unipe uvumilivu kama uliompa Nuh wakati anawaambia watu wapande meli kuna mafuriko yanakuja wakamcheka nisije mkata huyu mtu kofi lililonyooka likampandisha mashua na mafuriko yakamjia ndotoni akiwa kazimia, naomba unipe moyo wa huruma kama wa Adam kumsamehe Hawa baada ya kumlisha tunda nisije kumlisha ngumi akatembea kwenye garden nyuma ya nyumba yetu uchi, naomba unipe uwezo wa nabii Issa bin Mariam kunyanyua mikono juu na kushuka na samaki na mikate kwakua uongo wa huyu mtu umenipa njaa na ntakuja nimpasue sasaivi kama Samson alivyodondosha lijumba. Kwa hayo machache naomba usinipe nguvu ya kumuangalia maana kwa hii simu nimeshika ntamzabua kama Daud alivyomteremsha Goliath, AMINNNNNN..
.
By @idrissultan
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad