Shirikisho la Soka Tanzania TFF Wamjibu Zitto Kabwe Kuhusu Libya

Shirikisho la Soka Tanzania TFF limejibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuitaka Tanzania isusie kucheza mechi na Libya ili kupinga vitendo vya biashara ya utumwa inayoendelea nchini humo.

Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa suala hilo ni nyeti na limefikishwa katika uongozi wa juu na kwamba litatolewa majibu hivi karibuni.

“Msimamo utatolewa na viongozi wangu mara baada ya kukaa na kutafakari hali halisi kwa sasa, na wenye uwezo wa kukaa na kutafakari ni viongozi wa juu, itakapokuwa tayari mtajulishwa,” amesema Lucas

Jana, Zitto alitoa wito kwa TFF kuitaka timu ya Kilimanjaro Stars isusie mechi inayotarajiwa kuchezwa na Libya, ili kuonyesha kutokubaliana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuendeleza biashara ya utumwa.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mshauri wa Michezo nchini Zitto Zuberi Kabwe.... Tumeisikia na tunaitafakari rai yako.
    Zitto Zuberi Kabwe, Ukisha maliza Ziara nchini libya kutuletea hali halisi Tafadhali fanya Mkutano na Vijana wa Boda Boda hapa kwetu Manzese.
    Lini Unatarajia Kurudi toka Libya?

    ReplyDelete
  2. Jamani Mbona mnaniumizia Mwanangu..... Mshauri wa Michezo nchini ... Mpeni hata cha kufutia machozi.

    Mnaanika haya hapa chini.... Si mtamtia Uchizi asijielewe Huyu Dogo mdandia Mada. Itabidi amgoje Ufisini Mkuu Wa Mkoa Mh. Paul Makonda ili angalau amfikirie wazifa na Role stahiki.

    " Makonda, Bakhresa,IGP Sirro Wateuliwa Kwenye Kamati ya Maandalizi ya Fainali za AFCON U-17"

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad