MBUNGE wa Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema), Saed Kubenea amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa kuwa anataka kukihama chama hicho na kujiunga CCM, baada ya ‘kununuliwa’, amesema kamwe hatoshawishika kwa pesa kuhama chama hicho, na kwamba ataendelea kuwapigania wanachi wake akiwa ndani ya Chadema.
Kubenea ameyasema hayo leo Jumatano, Desemba 6, 2017 wakati akizungumza na wanahabri jijini Dar es Salaam kufuatia tetesi zilizosambaa mitandaoni kuwa anataka kukihama Chadema na kujiunga CCM kwa madai kuwa amenunuliwa kwa pesa na chama hicho.
“Baadhi ya magazeti ya leo yameandika yakinukuu kuwa nahama Chadema najiunga CCM, napenda niwahakikishie kuwa sijawahi kuongea na chombo chochote cha habari kuwa nina mpango wa kuhama Chadema, na kujiunga na chama kingine. Sijawahi kuzungumza na mtu yeyote wa CCM juu ya kujiunga na chama hicho.
“Nimekua mkosoaji mkubwa wa CCM juu ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma, uuzaji wa mashamba, nyumba za serikali na mengine…. sioni jipya linaloweza kunishawishi nikajiunga CCM. Mimi sijawahi kununuliwa na huwa sinunuliki, nikifanya jambo basi limetoka moyoni mwangu.
“Nimepata fursa ya kuwawakilisha wananchi, kutunga sheria bungeni, kamwe siwezi kuwasaliti wananchi wa Ubungo walionipigania hadi nikawa mbunge. Kuna watu nimewashawishi kuondoka CCM kuingia Chadema akiwemo Sumaye na Lowassa.
“Nimehudhunika, nimesikitika na nimeumia sana na taarifa hizo, mimi bado ni mwanachama wa Chadema na mbunge wa Jimbo la Ubungo hadi 2020 labda nife, nitaendela kuwa mwanachama mkweli na mwanimifu katika kukipigania chama changu, puuzeni huo uzushi wa mimi kuhama chama,” alisema Kubenea.
Akijibu maswali ya wanahabari kubenea alisema;
“Sina bei, bei yangu ni utu wangu, kinchofanyika ni propaganda za CCM ili asiulizwe kuhusu mambo mazito wanayoyafanya ikiwemo kuvunja jengo la Tanesco Ubungo wakati Ulaya kuna tereni zinapita chini ya bahari.
Aidha Kubenea ameeleza namna ambavyo uvumi wa yeye kuhama ulivyoanza kwenye grupu lake la WhatsApp kisha kusambaa kwenye mitandao na baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimeandika uongo pasipo kumuuliza.
Kwani vepe, si'tuliambiwa mnapigiwa simu na 'baba' kwamba munahitajika CCM kwa gharama yoyote!!! Au mnaogopa vivuli vyenu wenyewe tehetehetehe
ReplyDelete