HEADLINE inayobamba mitandaoni na kwenye vyombo vya ahabri kuanzia jana jioni ni kuhusu Malkia wa Filamu Bongo, Wema Sepetu kuhama Chadema na kutangaza kurudi kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo uamuzi huo umetolewa ufafanuzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akisema CCM haina taarifa za Wema kwani hajafuata taratibu kuanzia kwenye shina la chama na si kupitia mitandaoni.
“Chama chetu sio Daladala mtu anaweza kupanda na kushuka wakati wowote, ni heri akabaki hukohuko ama akaanzie kule ambako alichukulia kadi yetu,” aliandika Polepole.
Kauli hiyo imemuibua Staa wa Filamu aliyekuwa rafiki wa karibu wa Wema kabla hajahamia Chadema, Steve Nyerere ambaye amemtolea povu Polepole na kuijibu kauli yake hiyo akiandika;
“Hiki chama hujakiunda wewe wala kukianzisha wewe, umekikuta kama tulivyokikuta wote, kina waasisi wenye uchungu nacho na wako kimya.
“Wewe ni nani ukatishe watu moyo kukitumikia kama vile ndio unakimiliki, tulia polepole chama cha wote hiki, usilete ubinafsi kwenye kutumikia na kujenga ngome, hatuhitaji wenye cement na nondo tu, acha hata mwenye jiwe lake aweke kikubwa nyumba isimame, ni mchango pia” – aliandika Steve Nyerere.
Steve Nyerere Amvaa Polepole Kisa Wema Sepetu "Hiki Chama Umekikuta Kama Tulivyokikuta Wote"
2
December 02, 2017
Tags
Watu kabla ya kutema nyongo zao kwenye mitandao lazima watumie busara na kile wanachokisema. Mtu anajifanya mwana CCM alafu anathubutu kufunua kinywa chake nakuhoji Pole Pole ni nani? Jamani? Kila zama na wakati wake. Na kila wakati una watu wake. Kama kulikuwa na waasisi ndio lakini wenye zamana ya chama hivi sasa ni akina Pole Pole na ndio maana hata hao waasisi wamekaa kimya bila ya kusema lolote juu ya kauli au ufanisi wa muheshimiwa pole pole kwakuwa nafasi yake katika chama ni kubwa mno. Wewe Steven Nyerere kama nani kwenye CCM hata uhoji kauli ya katibu mwenezi na itikadi wa chama? Steven Nyerere lazima ujifunze adabu kwani ustaa wa bongo movie sio ustaa wa CCM. Wema alikikosea adabu chama ili kurudi ilim'bidi lazima aombe radhi na kufuata taratibu za chama hawezi tu akabadilisha chama kama anavyobadilisha wanaume ebo,CCM ni taasisi kubwa. Wakati umefika kwa watanzania kujifunza kukubali kuambiwa ukweli bila kujali yakuwa wewe staa au la. Pole Pole kwa kushirikiana na viongozi wenzake wa chama wanaifanya kazi kubwa mno kwenye chama hivi sasa kwa kweli sio haki atokezee mtu anaejifanya mwana CCM kumtupia maneno ya shombo kisa shoga yake kuulezwa ukweli lol.
ReplyDeleteLakini mie nnvyo Jua , Kweli huyu mdada anayo nia ya Kurudi nyumbani.
ReplyDeleteIsipokuwa Kule ni Mwenyekiti ndio katia Nanga kwake .. Sasa itakuwaje?
Na h
Haji Manara pia yuko Njiani kuchukua Jumla na isitoshe Hamolapa ameshaweka Bayana na Kuonesha Nia Hiyo Pia.
Mnavyo Shauri ni Bora kwanza amalize haya ya Muhimu halafu ndiyo Ya Vyama.
Amini usiamini hata Bila ya Kuwepo chama chochote akifanikisha hili basi ni poa Tu.
Kwani Wolper yuko chama gani?
CCM ni ile ile ... Mele kwa Mbeleeeeeee..