Tanzania Yaporomoka Viwango vya FIFA

Tanzania Yaporomoka Viwango vya FIFA


Tanzania imezidi kuporomoka kwenye viwango vya soka duniani baada ya kushuka kwa nafasi tano zaidi kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mwezi Novemba.

Orodha ya FIFA iliyotolewa leo ya viwango vya mwezi Novemba 2017, inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya 147 kutoka  142 mwezi Oktoba, ikiwa imeshuka kwa nafasi tano.

Wakati Tanzania ikishuka Uganda imeendelea kuongoza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ikiwa inashika nafasi ya 75 duniani huku Senegal ikiwa inaongoza kwa Afrika nzima ikiwa inashika nafasi ya 23 FIFA.

Kwa upoande wa 10 bora mwezi huu Ujerumani imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Brazil, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Hispania, Poland, Uswisi, Ufaransa na Chile.

Tanzania ilitoka sare ya 1-1 na Benin kwenye mchezo wa Kalenda ya FIFA kwa mwezi Novemba. Tanzania ilisafiri hadi Benin na kucheza katika uwanja wa l'Amitie mjini Cotonon.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad