Tanzia: Rais Wa Zamani wa Yemen Auwawa

Rais Wa Zamani wa Yemen Auwawa
Aliyekuwa Rais wa zamani wa Yemen, Ali Abdullah Saleh ameuawa katika mapigano na wafuasi wake wa zamani wa ‘Houthi’.

Mashirika ya habari nchini Yeman yanayodhibitiwa na waasi wa Houthi yamewanukuu maafisa polisi wakitangazakuwa mwisho wa mzozo wa wanamgambo wahaini na kiongozi wao umekwisha.

Chama cha Saleh cha General People’s Congress (GPC) kimethibitisha taarifa cha kifo cha kiongozi wao kupitia kituo cha runinga cha Al Arabiya TV cha nchini Saudi Arabia.

Picha na video zilizosambazwa mtandaoni zimeuonesha mwili wa mwanamume anayesadikika kuwa ni Bw. Saleh ukiwa na kidonda kwenye paji la uso wake.

Hadi kufikia wiki iliyopita, wafuasi wanaomuunga mkono Bw. Saleh walikuwa wanapigana na wapiganaji wa jamii ya Houthi ambao zamani walikuwa wanamuunga mkono Bw. Saleh dhidi ya Rais wa sasa wa Yemen, Abdrabbuh Mansour Hadi.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa (U.N) Watu zaidi ya 8,670 wameuawa na wengine 49,960 kujeruhiwa tangu majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yalipoingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2015.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad