Shirikisho la Soka Tanzania TFF limejibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuitaka Tanzania isusie kucheza mechi na Libya ili kupinga vitendo vya biashara ya utumwa inayoendelea nchini humo.
Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema suala hilo limefikishwa kwa uongozi wa TFF na litatolewa majibu hivi karibuni.
"Msimamo utatolewa na viongozi wangu mara baada ya kukaa na kutafakari hali halisi kwa sasa, na wenye uwezo wa kukaa na kutafakari ni viongozi wa juu, itakapokuwa tayari mtajulishwa", amesema Alfred Lucas.
Hapo jana Zitto Kabwe ametoa wito kwa TFF kuitaka timu ya Kilinajaro Stars isusie mechi inayotarajiwa kuchezwa na Libya, ili kuonyesha kutokubaliana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuendeleza biasha ra utumwa.
Pia umoja wa nchi za Africa uiwekee vikwazo Libya. Africa tuwe na sauti moja against slavery trade. Kamwe tusiliache tatizo kukua na Kuota mizizi, kwani itakuwa ngumu kulitokomeza km ilivyokuwa ngumu kutokomeza ubaguzi wa rangi na utawala wa kigeni kusini mwa Africa. Had Leo ndugu zetu weusi wa kiamerica wamekosa identity. Wanabaguliwa na kuuawa na wanaonekana sio originally wa America. Na mbaya zaidi hata huku Africa walikotokea kamwe hatujawahi kuwaona ni wenzetu na ndugu zetu hasa wa damu. Ila tuna wa identify km wa America. Kamwe sijasikia AU unequivocally ikipinga Mauaji yao au manyanyaso yao. Sijasikia AU ikidiscus au kuwatangazia 'wanetu rudini nyumbani na huku Africa ndo kwenu'
ReplyDelete