TFF Yawakingia Kifua Kilimanjaro Stars "Wachezaji Walibadili Jezi Airport"

TFF Yawakingia Kifua Kilimanjaro Stars "Wachezaji Walibadili Jezi Airport"
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesikitishwa na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kwamba wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ walirudi nchini jana bila ya kuwa kwenye sare na badala yake kila mmoja alivaa nguo zake binafsi.

Taarifa hizo si za kweli na zimelenga kuwapotosha wa Tanzania na wapenda mpira wa miguu ama kwa makusudi au kwa sababu binafsi kwa wale wanaosambaza taarifa hizo.

Kilimanjaro Stars ilitua nchini saa 2.30 asubuhi kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) wachezaji wote wakiwa ndani ya sare.

Baadhi ya wachezaji waliomba kwa uongozi kwamba hawana mpango wa kwenda kambini badala yake walitaka kwenda kuungana na familia zao ambazo zilifika uwanjani kuwalaki. Uongozi uliwakubalia na hivyo kupata eneo la faragha Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ili kubadili sare husika na kuvaa nguo binfasi za kawida kabla ya kutawanyika.

Wachezaji walibadili sare hizo baada ya kufanyika utaratibu wote wa kuvunjwa kwa kambi na kwa kuwa kila mmoja alikuwa anarudi nyumbani kwake alikuwa na uhuru wa kuvaa mavazi anayoyataka.

TFF inachukuwa nafasi hii kukanushana kulaani taarifa hizo ambazo hazikuzingatia uweledi wa kuuliza upande wa pili na tunasisitiza kuwa wachezaji walirudi kila mmoja akiwa kwenye sare maalumu za timu kwa kuwa TFF siku zote tunaamini katika utaratibu na tumekuwa waumini wazuri wa kufuata utaratibu tunaojiwekea.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hyo sio issue wavae wasivae haituhusu, issue kwa nini wamecheza kama Zanzibar aka mdebwedo hrf Zanzibar ndio wanakaza ssa kama bara

    ReplyDelete
  2. Hyo sio issue wavae wasivae haituhusu, issue kwa nini wamecheza kama Zanzibar aka mdebwedo hrf Zanzibar ndio wanakaza ssa kama bara

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad