Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Timbulo amesema wasanii wa Bongo wajifunze kutoa kazi zao kwa lengo la kujitangaza nje ya nchi kuliko kutengemea wasanii wa nje ambao muda mwingine hawana mchango wowote.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Vibaya’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa mfano mzuri kolabo ya Diamond na Davido kwani kolabo hiyo ilimtangaza zaidi Davido hapa nchini kuliko Diamond nchini Nigeria.
“Kumshirikisha msanii wa nje ni kumleta hapa, tumemjua Davido baada ya kushirikishwa na Diamond baada hapo Davido alikuwa kama Mtanzania vile, anavyopingwa utasema anatokea Manzese vile lakini Davido hakumsaidia kule. Chukua mziki upeleke kule, Darassa ame-trend mpaka Afrimma hakumshirikisha msanii yeyote wa nje” amesema Timbulo.
Timbulo aliendelea kwa kusema Alikiba ameweza kushinda tuzo bila kolabo na msanii wa nje na kueleza hivyo ndivyo inatakiwa.
“Mfano Turudi hapa hapa, Alikiba amefanya kazi nyingi na amefikia hatua amechukua tuzo za MTV si kwa kolabo ni kazi za nyumbani, kwa hiyo tunaweza kufanya siyo lazima kolabo nje watu wasikariri” amesisitiza.