TRA Kumchunguza Askofu Kakobe Baada ya Kumsikia Akisema ana Hela kuliko Serikali

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema;

Watu wa Kodi (TRA) wanasema wamepokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao

TRA wanaendelea na kusema; Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema

Hivyo Askofu Kakobe ni tajiri sana kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TRA wanasema wanawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe wakaanza kupitia kumbukumbu zao ili kuona namna Askofu Kakobe anavyolipa Kodi. Wanasema alipitia na kuona Kuwa Kakobe aliyesema anaizidi Serikali kwa pesa hakuna kumbukumbu za ulipaji kodi wake.

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere anaendelea na kusema;

"Kuna Matajiri tunawafahamu lakini hawaizidi serikali kwa pesa, tumeona wamekuwa wakilipa kodi na kuonekana kwenye kumbukumbu zetu lakini huyu tajiri Askofu Kakobe si miongoni mwao. Hivyo basi sisi watu wa Kodi tunataka tujiridhishe tu kuhusu swala la kodi kuhusiana na Askofu Kakobe na utajiri wake"

"Sisi Wataalamu wa mambo ya kodi tutafahamu tu kama utajiri wake anaousema unatokana na sadaka tu au kuna shughuli nyingine za kiuchumi anafanya"

"Tunaelewa kwa mujibu wa sheria sadaka haitozwi kodi, ila tunafahamu taasisi za dini huwa zina shughuli nyingine za kiuchumi, huenda Askofu Kakobe na yeye akawa na shughuli nyingine zinampatia hela mpaka akawa na pesa nyingi kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

"Lakini pia kama kweli ni sadaka pekee inayomfanya Askofu Kakobe awe na pesa nyingi kuliko Serikali ni jambo la kushtua kidogo. Basi hizo sadaka ni nyingi kweli kweli na watoa sadaka watakuwa matajiri kweli kweli"

Mwisho TRA wamtaka Askofu Kakobe kutoa ushirikiano ili wajiridhishe juu ya utajiri wake na ulipaji kodi


Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli ni tajiri na utajiri huo ameupata kwa kuwadhulumu waumini wake kwa malimbuko ya aina mbalimbali ikiwemo mikufu ya dhahabu. Malimbuko hayo ndo yanamtia kiburi

    ReplyDelete
  2. Inawezekana pia kakobe anatumia taasisi yake ya dini kujihusisha na biashara ya haramu ya madawa ya kulevya au hata human trafficking inapaswa achunguzwe haswa.

    ReplyDelete
  3. Tena kwa kina... Manake baada ya kukaa kwa kimvuli miaka nenda miaka rudi. halipi kodi na tuememwachia mpaka yeye mwenyewe anafunguka.
    Hili ni jambo si la mzaha. Kodi ni lazima aitoe na atozwe na wengine wengi tu ambao wako nyuma ya Taasisi kama hizo.
    Kakobe wewe is mwana dini bali ni Mbwa mwitu alie vaa ngoxi ya kondooo. Lakini sasa hivi umejifichua mwenyewe na wamaume wataingia kazini mpaka kijulikane.
    Msigwa alikua anauliza Viongozi wa dini mko wapi?
    sasa we amekuponzaaaa. TLA Mahakama Tukukulu wote wako njiani Kakobe. Na Bila ya kumsahau Sirro.

    ReplyDelete
  4. We need to protest and let the Vatican know...!!!!
    We cannot tolerate this kind on behaviour from such Top post from the Church.
    We can then wecome him thru Political parties ( NCCR or TLP or Act. But not the church being turned a political Platform.

    ReplyDelete
  5. We need to protest to the Vatican to the Pope. and let the Vatican know Church being turn as a political portfolio...!!!!
    We cannot tolerate this kind on behaviour from such Top post from the Church.
    We can then wecome him thru Political parties ( NCCR or TLP or Act. But not the church being turned a political Platform.

    ReplyDelete
  6. Kakobe itakula kwako....Hivi wewe ni wa wapi?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad