Majaji wa Ufaransa wamemaliza upelelezi juu ya shambulio la kombora ambalo lilisababisha kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.
Ofisi ya mwendesha mashitaka sasa wataamua ikiwa waipeleke kesi mbele ya mahakama. Majaji wamewalaumu wapiganaji walioongozwa na rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame kwa kuilenga na kuiangusha ndege iliyokuwa imembeba rais wa wakati huo wa taifa hilo, Juvenal Habyarimana.
Rwanda nayo inawalaumu Ufaransa kwa kushiriki kupanga mauaji ya kimbari. Upelelezi umesababisha sintofahamu kati ya mataifa haya mawili, kiasi cha Rwanda kuvunja uhusiano wa kidplomasi a na ufaransa mwaka 2006.
Uhusiano huo ulirejeshwa miaka mitatu iliyopita.