Uhamiaji Kutoa Ukweli Kuhusu Askofu Niwemugizi Baada ya Uchunguzi Kukamilika

Uhamiaji Kutoa Ukweli Kuhusu Askofu Niwemugizi Baada ya Uchunguzi Kukamilika
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala amesema uchunguzi utakapokamilika wataweka wazi sababu za kuhoji uraia wa Askofu wa Jimbo la Ngara - Rulenge, Severine Niwemugizi.

Dk Anna amesema hayo baada ya kuhojiwa na Mwananchi leo Jumatano kwa njia ya simu kuhusu sababu za kufanya mahojiano kuhusu uraia wa Askofu huyo.

“Hizo ni taarifa za kiuchunguzi, ambazo bado tunaendelea, huwezi ku-disclose kila kitu hata tunayemuhoji hatutakuwa tunamtendea haki, tunapokuwa na doubt ya uraia tunaruhusiwa kuchunguza,” amesema Dk Anna.

Alipoulizwa kuhusu madai ya msimamo wa Askofu Niwemugizi kuhusu Katiba mpya ndiyo pengine umesababisha kuhojiwa uraia wake, Dk Anna amesema hakuna haja ya kueleza chochote kuhusiana na madai hayo hivyo ni vyema kusubiri taarifa za uchunguzi wake.
Chanzo: Mwanamchi

“Hayo ni yake, sitaki kuongelea hilo, hayo tuyaache,” amesema.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera Mama Anna. Fanya kazi yako as Mandated.
    Imani na wewe Tunayo tena Kubwa Sana.

    Watu wengi wa Ruhengeri walia hamia Rulenge kwa muda Tofauti.
    Uhakiki unao ufanya ni Wajibu na Ni Halali.
    Tanzania Yetu ni Salama na Amani.
    Hatuto kubali waka Kunyamaza ikiwa kuna Jambo la Sivyo ndivy and Watu wa Hapa Kule Hatuwataki.

    Endelea na Upembuzi wako Mama mpaka Uridhike kwa Uzalendo wako na Amani ya Nchi yako.

    Hapa Kazi Tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad