Umati Wamuokoa Rais wa Zamani wa Georgia Kutoka kwa Polisi Ukrain

Umati Wamuokoa Rais wa Zamani wa Georgia Kutoka kwa Polisi Ukrain
Wafuasi wa rais wa zamani wa Georgia Mikheil Saakashvili wamemoukoa kutoka kwa gari la polisi kwennye mji mkuu Kiev baada ya kukamatwa kufuatia madai kuwa anasaidia kundi la kigaidi.
Bw Saakashvili 49, aliutaka umati kumuandoa madarakani rais Petro Poroshenko ambaye ni mshirika wake wa zamani.
Alipewa uraia wa Ukrain mwaka 2015 hatua iliyosababisha apoteze uraia wake wa Georgia.
Rais wa zamani wa Georgia aingia Ukrain kwa nguvu
Bw. Saakashvili amekuwa mkosoaji mkubwa wa Bw. Poroshenko.
Anamlaumu rais kwa kushindwa kumaliza ufisadi. Bw Porokoshenko amekana madai kama hayo hapo awali.
Georgian former President Mikheil Saakashvili flashes a victory sign after he was freed by his supporters in KievHaki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Umati wamuokoa rais wa zamani wa Georgia kutoka kwa polisi Ukrain
Akiwa na pingu kwenye mkono mmoja na akizungukwa na mamia ya watu, Bw Saakashvili aliwashauri wafuasi wake kutembea kwenda kwa bunge la Ukrain.
"Ninawashauri kuanza maandamano ya amani ya kumuondoa madarakani Poroshenko. Msiogope," alisema kwa njia ya vipasa sauti.
Ukrain: Urusi ilihusika na udukuzi wa mitandao
Maafisa hawazungumzi lolote kufuatia kukombolewa kwa Bw Saakashvili. Mapema maafisa waliokuwa wamejifunika nyuso walimkamata Bw. Saakashvili, 49 kutoka nyumbani mwake.
Bw Saakashvili anashukiwa kwa kupokea msaada ya kufedha kutoka kwa kundi lenye uhusiano na rais wa zamani wa Ukrain Victor Yanukovich.
Bw. Saakashvile anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano jela ikiwa atapatikana na hatia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad