Umoja wa Mataifa (UN) Yathibitisha Kuuwawa kwa Wanajeshi 12 wa Tanzania Congo


Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa takribani wanajeshi 12 kutoka Tanzania waliokuwa wanalinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo (DRC) wameuawa na wengine 53 kujeruhiwa vibaya baada ya kambi yao kuvamiwa na waasi mapema leo.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kupitia mtando wa Twitter imeeleza.

“Taarifa za awali katika eneo la shambulio mjini Kivu Kaskazini zinaonesha kuwa takribani walinda amani 12 kutoka Tanzania wameuawa  na wengine 44 kujeruhiwa vibaya.“amesema Guterres.

Bw. Guterres amesema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni huku akielezwa kusikitishwa na tukio hilo.

“Ningependa kueleza kusikitishwa kwangu na shambulio hilo lililotekelezwa usiku wa jana dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Shambulio hilo lilitekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo.

“Natuma salamu zangu za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa wanajeshi wa kulinda Amani na wanajeshi wa FARDCwaliouawa au kujeruhiwa,” amesema mwakilishi mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo ambaye ndiye pia mkuu wa kikosi cha walinda amani cha MONUSCO.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad