Utafiti: Kunywa Glasi Moja ya Wine Kila Siku Kuna Manufaa Haya


Utafiti: Kunywa Glasi Moja ya Wine Kila Siku Kuna Manufaa Haya

Utafiti wa siku za hivi karibuni uliofanywa na wanasayansi wa nchini China umeonesha kuwa kunywa glasi moja ya mvinyo yaani ‘wine’ kila siku hupunguza hatari ya kifo cha mapema kwa mara tano.

Wanasayansi hawa pia wameeleza kuwa kukiuka unywaji huu unaoshauriwa kiafya kwa kunywa zaidi hatari ya kifo inaongezeka kwa asilimia 11 ikiwa ni pamoja na kuongeza hatari ya kufa kwa magonjwa ya saratani kwa asilimia 27.

Inaelezwa kwa matunda ya zabibu yanayotumika kutengeneza wine huwa na virutubisho vijulikanavyo kama ‘resveratrol’ ambavyo huongeza na kuboresha afya ya moyo, kusaidia kutoa kinga ya magonjwa ya saratani na kulinda macho dhidi ya uoni hafifu

Kwa mujibu wa Mwandishi Mkuu wa utafiti huo Professor Bo Xi, japokuwa unywaji wa kiasi husaidia kupunguza magonjwa yanayohusiana na moyo unywaji wa kupitilza huweza kusababisha kifo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad