Hapo nyuma, Vanessa Mdee aliwaahidi mashabiki zake kuwa , kabla ya mwaka huu 2017 kuisha, atatoa Albamu yake yenye nyimbo18 ambayo itakuwa imewashirikisha wasanii wa Tanzania na nje ya Tanzania.
Kupitia mtandao wake wa Instagram Vanessa Mdee ameonyesha kava ya albamu hiyo (Muonekano) na kuthibitisha hiyo ndio yenyewe kwa kuandika,
"This is the official album cover #MoneyMondaysTheAlbum".
Tusubiri tarehe rasmi ya albamu hiyo na kuweza kuwafahamu zaidi watu aliowashirikisha katika Albamu hiyo